ROYA GARDEN LODGE MSAMVU WAMEPATA OFFER YETU!

 
Mustapha Madish Installers Morogoro bado tupo kwenye offer kwenye huduma zetu zote iwe mifumo ya ulinzi, mifumo ya tv ama mambo mengine ya ICT!

Tupo kwenye Door to Door kwa wale wateja wetu walengwa nikiwa na maana majengo yaliyojengwa na yanayojengwa iwe Hotel,  Lodge,  Apartment, Office,  Industries n.k.

Tulipata wasaa wa kupita Roya Garden lodge maeneo ya Msamvu na kwenye kuwafafanulia huduma na offer zetu ndipo wakatueleza shida zao, ilikuwa upande wa mfumo wa TV, kuna tv ambazo hazina signal, kuna tv ambazo hasiwaki kabisa na kuna tv ambazo hazihifadhi channels yaani signal ipo ukisearch channels zinaingia lakini tv ukiizima na kuiwasha channels zinapotea mpaka kusearch tena!

Tukaangalia tatizo, tukampa bei baada ya kupunguza 10% kisha tukafanyakazi safi na kukabidhi kazi tukalipwa ujira wetu tunashukuru na kuaga!🤝🏾

Kama upo Morogoro na hatujakufikia bado tupigie namba zetu ni +255777139413

Post a Comment

0 Comments